Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Marcio Maximo ametambulishwa kama kocha mkuu mpya wa klabu ya KMC FC akichukua mikoba ya Kally Ongala aliyetupiwa virago mwezi Mei kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo.
Maximo (63) raia wa Brazil ambaye pia amewahi kuinoa Young Africans Sc anakumbukwa zaidi kwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu Michuano ya CHAN kwa mara ya kwanza mwaka 2009.
Comments