MWEGELO APENDEJEZA KUANZISHWA KWA TAMASHA LA VIJANA WA VYAMA VYA UMOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM TAIFA), Jokate Mwegelo, amepata heshima ya kipekee kwa kuteuliwa kuwasilisha mapendekezo ya vijana wa vyama vya ukombozi kutoka Kusini mwa Afrika katika mkutano wa kimataifa uliowakutanisha wanachama wa vyama hivyo pamoja na wageni kutoka mataifa mbalimbali nje ya Afrika.

Kupitia taarifa aliyoandika kwenye mitandao ya kijamii, Jokate amesema alipata nafasi hiyo adhimu kutokana na imani kubwa waliyoionyesha viongozi wenzake kutoka vyama rafiki vya ukombozi.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa heshima na wageni waalikwa, na katika mjadala ulioshereheshwa na Katibu Mkuu wa ANC, Comrade Fikile Mbalula, Jokate aliwasilisha mapendekezo mbalimbali ya vijana, likiwemo wazo kuu la kuanzishwa kwa Tamasha la Vijana wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (Liberation Movement Youth Festival).

Tamasha hilo linalopendekezwa litawakutanisha vijana kutoka Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji, Zimbabwe, Angola na Namibia kwa ajili ya kufanya mijadala ya kisiasa, kubadilishana uzoefu wa kiuongozi na kujadili fursa mbalimbali za kiuchumi.

Kwa mujibu wa Jokate, pendekezo hilo limepokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa vyama husika na sasa hatua inayofuata ni utekelezaji rasmi wa wazo hilo la kihistoria.
"Ni furaha ilioje kwamba pendekezo hili limekubaliwa, na hivyo imebaki utekelezaji. Asanteni kwa imani kubwa mlionionesha, vijana wenzangu wa Afrika," ameandika @jokatemwegelo

Akihitimisha ujumbe wake, Jokate alieleza mshikamano wake na harakati za vijana kwa maneno maarufu: “Aluta Continue, Amandla, Viva Vijana Viva!”







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...