TANZANIA YAANZA VYEMA CHAN2024 YAIPIGA BURKINAFASO 2 KWA NUNGE

TANZANIA imeanza vyema Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo wa Kundi B usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao Taifa Stars yaliyoizamisha The Stallions yamefungwa na kiungo mshambuliaji, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ wa Azam FC kipindi cha kwanza na beki Mohamed Hussein Mohamed ‘Tshabalala’ wa Simba SC kipindi cha pili.

Sopu alifunga bao lake kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45’+3 baada ya mshambuliaji Clement Francis Mzize kuangushwa kwenye boksi na beki wa USFA, Franck Aimé Tologo kufuatia pasi ya mchezaji mwenzake wa Yanga, kiungo Mudathir Yahya Abbas.

Naye Tshabalala anayejulikana kama Zimbwe Junior kwa jina lingine la utani alifunga bao lake kwa kichwa akimalizia krosi ya winga wa Azam FC, Iddi Suleiman Ali ‘Nado’ dakika ya 71, ingawa ilibidi refa Lotfi Bekouassa wa Algeria ajiridhishe kwa Marudio ya Picha za Video (VAR).
Baada ya mchezo huo, kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ alikabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi.





 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

DUNIA NI KATILI SANA KWA MWANAUME MASIKINI

MWANAUME USIPITWE NA HILI, INASIKITISHA...?!!!

USAJILI ULIVYO HADI SASA....

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KUOA

RAIS SAMIA AYATAKA MASHINDANO YA MISS WORLD 2027

MAMBO 7 MUHIMU YA KUYAEPUKA BAADA YA KUACHANA...