Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa mkoani Ruvuma ameahidi kutekeleza mradi mkubwa wa barabara ya kilomita 512 kutoka Lumecha – Londo – Malinyi – Lupiro, barabara inayounganisha mikoa ya Ruvuma na Morogoro.
Serikali tayari imesaini mkataba na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa mfumo wa “Design & Build” – njia ya kisasa inayohakikisha ujenzi wa haraka, ubora na viwango vya kimataifa.
Barabara hiyo si tu itarahisisha usafiri na biashara, bali pia itafungua fursa mpya za kiuchumi, kijamii na maendeleo kwa mikoa yote miwili na taifa kwa ujumla.
Hatua hii ni kielelezo cha dhamira ya Tanzania kuwekeza kwenye miundombinu ya kimkakati ili kuunganisha watu, kuongeza uchumi na kuimarisha ushindani wa kitaifa na kimataifa.
muonekano wa barabara eneo la Kitanda kwenda Londo,pia muonekano wa kiijiji cha Kitanda wilayani Namtumbo ambako barabara hiyo ya kimkakati inapita kuunganisha na Mkoa wa Morogoro
Comments