Na Richard Mwaikenda, Songea
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga stendi kubwa ya malori,Soko kubwa la mazao katika Jimbo la Mchinga mkoani, Lindi.
Dkt. Samia ametoa ahadi hizo katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika Jimbo la Mchinga leo Septemba 25, 2025. Jimbo hilo linaongozwa na Salma Kikwete mke wa Rais mstaafu, DKT. Jakaya Kikwete.
Aidha, Rais Dkt. Samia ameahidi kutuma wataalamu watakaofanya tathmini ya uanzishaji wa kiwanda Cha kuchakata zao la mwani ili kukiongezea thamani.
Katika mkutano ameahidi kwamba endapo wananchi watampatia ridhaa z tena Nchi kwa ukimpigia kura katika Uchaguzi Oktoba 29,2025 atahakikisha anakamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya miundombinu ya barabara, afya, maji na nishati.
Katika mkutano huo kujinadi yeye, Mgombea ubunge wa jimbo la Mchinga, Salma Kikwete na madiwani na kujibu maombi hayo ya Salma.
Akiwa katika mikutano hiyo, Dkt. Samia anajinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika mikoa hiyo, pia kutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Aidha, Dkt. Samia amekuwa akisisitiza kudumisha Muungano na kuendelea kulinda amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, ambapo pia amewatoa wananchi wasiwasi kwamba hakutokuwa na vurugu kwani vyombo vyote vya ulinzi viko imara, hivyo siku ya Uchaguzi Oktoba 29 mwaka huu amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi tena bila hofu kwenda kupiga kura na kurejea salama majumbani.
Vilevile Dk.Samia ameendelea kuwahamasisha wananchi kwamba ikifika siku ya kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu waende kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni yeye, wabunge na madiwani wa Chama hicho ili kasi ya kuleta maendeleo ya watanzania iendelee.
Pamoja na kuelezea kwa undani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. Emmauel Nchimbi, atatumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho.
Comments