DKT. SAMIA AIPONGEZA PWANI KWA KASI KUBWA YA MAENDELEO

‎Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Samia Suluhu Hassan ameupongeza mkoa wa Pwani  kwa kasi kubwa ya maendeleo ya viwanda ambapo idadi imeongezeka kutoka viwanda 1,587 hadi viwanda 1,631 kwa mwaka huu.

‎Amesema kuwa  ongezeko hilo sawa na ongezeko la viwanda 244 ndani ya miaka minne au viwanda 61 kila mwaka.

‎Amefafanua kuwa viwanda vya kati 81 vimejengwa ambapo sasa vimefikia 161 sawa na viwanda 26 kila mwaka na kwamba vimetoa ajira za moja kwa moja 21,146 na zisizokuwa za moja kwa moja ajira 60,000.

‎Amepotoa pongezi hizo katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya Sabasaba Kibaha mkoani Pwani Septemba 28,2025.

‎“Hapa sijavitaja viwanda vidogo ambavyo vimewanufaisha Watanzania wengi kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.Uwekezaji uliofanyika umewezesha nchi yetu kupiga hatua kujitegemea kimapato na bidhaa.

‎“Kwa mfano  ndani ya Mkoa wa Pwani kuna uzalishaji mkubwa unaofanya nchi ijitegemee kwenye bidhaa muhimu.”Sasa tunajitegemea kwenye uzalishaji vioo lakini marumaru, saruji, mabati ya rangi vyote vinazalishwa ndani ya nchi."

‎Pia Dk. Samia amesema  kutokana na kasi kubwa ya ukuaji viwanda serikali imeamua kujenga vituo vya kupoza umeme eneo la Msufini Mkuranga kwa gharama ya sh. bilioni 388.3.

‎“Kituo kingine kitajengwa Zegereni Kibaha kwa gharama ya sh. bilioni 54.7 na Zinga Bagamoyo kwa sh. bilioni 120.Umeme huo utakuwa wenye uhakika kuufanya mkoa huo kutokumbwa na upungufu wa umeme, hivyo viwanda vitazalisha muda wote.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

LEO NI LEO KAMPENI ZA DKT. SAMIA SONGWE

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-