KANDA YA KASKAZINI WAAHIDI KUMPA DKT. SAMIA KURA ZA KUSHAMGAZA


Wananchi wa Kanda ya Kaskazini wameahidi kumpatia kura za kishindo  zitakazomshangaza kila Mtu, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.


Ahadi hiyo imetolewa kwa niaba wananchรญ na  Frederick Sumaye Waziri Mkuu mstaafu, ambaye ni mratibu wa Kanda hiyo katika mkutano wa Kampeni za CCM wilayani Same Septemba 30, 2025. Kanda hiyo inajumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.


"Kanda hii ya kaskazini sehemu zake zingine kwa kawaida hazikuwa nzuri sana kwa CCM huko miaka ya nyuma, wananchi wa Kilimanjaro wanataka kufuta historia hiyo kwa kukupa wewe Dkt. ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—น๐˜‚๐—ต๐˜‚ ๐—›๐—ฎ๐˜€๐˜€๐—ฎ๐—ป kura nyingi sana na kupata ushindi wa kishindo ambao haujawahi kutokea"


"..wananchi wa kilimanjaro wameamua, wanakupenda na watakupa kura nyingi sana.."


"..sisi wasaidizi wako tumezunguka maeneo mbalimbali ya majimbo kilimanjaro..wananchi wengi wanatamka yale uliyowafanyia katika kuleta maendeleo na hakika umeacha alama na ndio maana wamekusudia kukuchagua wewe ifikapo Oktoba 29 katika uchaguzi mkuu."


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

LEO NI LEO KAMPENI ZA DKT. SAMIA SONGWE

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM