Kongole Shujaa na Bingwa wa Dunia wa Marathoni Sajinitaji @simbualphonce kwa kupandishwa cheo kutoka Sajini (Sergeant) na kuwa Sajinitaji (Staff Sergeant) ikiwa ni kutambua mchango wako mkubwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Tanzania na Afrika kwa ujumla katika kuendeleza michezo na kuiletea Tanzania heshima Kimataifa.
Asante CDF Jacob John Mkunda kwa mchango mkubwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika michezo na kuwatia moyo wanamichezo.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tutaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano tulionao katika kuendelea michezo Kitaifa na Kimataifa.
Comments