Na Richard Mwaikenda, Lindi
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewakikishia Wananchi wa Mkoa wa Lindi kwamba mradi mkubwa wa gesi asilia aina ya NLG wenye thamani ya sh. bil. 40 uko mbioni kuanza.
Ametoa uhakika huo alipokuwa akihutubia katika mkutano wa Kampeni za CCM kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi Mjini Septemba 25,2025.
Amesema kuwa wapo katika hatua za Mwisho za makubaliano na mwekezaji wa mradi huo ili kila upande ujue utafaidikaje na mradi.
"Mradi wa bil. 40 ni mkubwa, Mwekezaji lazima awe na uhakika, nasi pia tuwe na uhakika tutapata nini kupitia rasilimali yetu hiyo. Tupo hatua za mwisho za makubaliano. Mradi upo na utaanza, ndiyo maana Chuo kinaendelea kujengwa ili vijana wetu wapate ajira, " ametoa uhakika huo Dkt. Samia.
Comments