UWANJA WA NDEGE WA KISASA KUJENGWA LINDI,AHADI YA DKT. SAMIA


 ‎UWANJA wa ndege mkubwa wa njia tatu za kuingilia na kutoka utajengwa mkoani Lindi.


‎Hayo, yamebainishwa na Waziri Mkuu,  Majaliwa Kassim Majaliwa alipokaribishwa kutoa salamu zake katika mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt.. Samia Suluhu Hassan kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi Mjini.


‎Mradi huo wa aina yake na miradi mingine mingi ukiwemo wa gesi aina ya NLG imo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM inayonadiwa na DKT. Samia katika kampeni za CCM zinazoendelea nchini.


‎Miradi mingine mikubwa inayotekelezwa mkoani humo ni; ujenzi wa Bandari ya uvuvi ya kimataifa ya Kilwa, Ujenzi wa ukuta ufukweni, ujenzi wa Chuo Cha VETA na kuifanyia maboresho makubwa Barabara Kuu ya Kibiti Lindi.


‎Dkt. Samia amemaliza Kampeni zake katika mkoa huo jana Septemba 25, 2025 kwa kufanya mikutano Ruangwa, Mtama na Mchinda.


‎Leo anaendelea na kampeni zake Mjini Mtwara.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

LEO NI LEO KAMPENI ZA DKT. SAMIA SONGWE

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-