Bwana John Shepherd Barron ameingia kwenye vitabu vya historia akiwa kama ni mvumbuzi ATM machine ya kwanza duniani mnamo tarehe 27 juni mwaka 1967. Ambapo ATM machine ya kwanza kabisa iliwekwa Barclays Bank London.
Moja ya kitu ambacho kinavutia kwenye simulizi yake kuelekea kwenye uvumbuzi wa ATM machine ni kwamba siku moja bwana John Barron alikuwa ana uhitaji wa kutoa pesa. Lakini bahati mbaya ni kwamba alichelewa kufika benki hivyo akakuta benki tayari pameshafungwa. Kutokana na kwamba alikuwa ana uhitaji sana na hela kwa wakati huo Bwana John alikasirika mno.
Na ndipo akapata wazo ya kwamba kwanini pasiwepo na kifaa ambacho kitatuwezesha watu kupata pesa zetu hata kama benki zitakuwa tayari zimefungwa ? Yani alihitaji kila mtu awe na uhakika wa kupata hela yake anapoihitaji ndani ya masaa 24. Na ndipo alipokuja kupata wazo la kutengeneza ATM ( Automated Teller Machine).
Mwanzoni kabisa namba ya siri ikiyokuwa ikitumika kwenye ATM ilikuwa na tarakimu 6. Lakini mkewake Bi.Caroline alimshauri kwa kumwambia kuwa tarakimu 6 ni nyingi sana haitokuwa rahisi kwa mtu kukumbuka. Ni vyema angalau ukaweka tarakimu hata nne. Na hapo ndio ukawa mwanzo wa kutumia tarakimu nne kwenye namba zetu za siri za kwenye ATM.
✍️ @thiago_technenga
Comments