Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga Mji wa AFCON City Arusha utakaotumika wakati wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika Mwaka 2027.
Amesema kuwa Mji huo wenye hadhi utajengwa karibu na Uwanja mpya wa soka wa Samia wenye uwezo wa kuingia mashabiki 32 kwa mkupuo.Michuano hiyo itafanyika Tanzania, Kenya na Uganda.
Aidha. Dkt. Samia amesema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu, Serikali anayoiongoza itanunua ndege nyingine 8 kwa lengo la kukuza zaidi sekta ya utalii.
Pia katika kipindi chake cha uongozi wa miaka minne na ushee wameufanyia matengenezo makubwa uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisonge ambao hivi sasa ndege zitakuwa zinatua usiku na mchana.
Lakini vile vile wanaendelea kujenga Uwanja wa ndege wa Karatu.
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi dkt. Samia.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, na Mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye akieleza sababu zilizoifanya NEC kumpitisha Dkt. Samia kuwa mgombea urais wa chama hicho.
Comments