Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amewaeleza wananchi wa Shinyanga kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita serikali ya awamu ya sita imeongeza utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo wa madini hadi kufikia 1766 kutoka leseni 332 kama ilivyokuwa mwanzo.
Ameyasema hayo wakati akijinadi kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika Maganzo, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga leo tarehe 11 Oktoba 2025.
Dkt. Samia amewapongeza wachimbaji wadogo wa madini ya Almasi katika eneo hilo pamoja na wachimbaji wote wadogo nchini kwa bainisha kuwa wameweza kuchangia asilimia 40 ya pato la madini nchini.
Pia, Dkt. Samia ameahidi iwapo wananchi wataendelea kukichagua Chama Cha Mapinduzi, kupitia Serikali yake ataendelea kuimarisha sekta ya madini nchini kwa kutoa kipaumbele zaidi kwa wachimbaji wadogo.
Aidha, Amebainisha kuwa anafahamu kuhusu mgogoro uliopo katika Wilaya hiyo baina ya wamiliki wa mgodi, wananchi na wachimbaji wadogo kwa kuwahakikishia kuwa hatua zinachukuliwa na mgogoro huo utatatuliwa vema.
Aidha, akigusia kuhusu miundombinu ya barabara, Dkt. Samia ametangaza kuijenga upya barabara ya Kolandoto- Mwangongo, Manispaa ya Shinyanga kwa kiwango cha lami, mara baada ya kuwa inafanyiwa ukarabati wa mara kwa mara kwa muda mrefu.
Huu ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni ndani ya mkoa wa Shinyanga aliyoianza leo mkoani humo.
Comments