Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻, ameahidi kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ili kuboresha mtandao wa barabara Jijini Mwanza na kuhakikisha zinajengwa kwa viwango vinavyokubalika kwa maana ya lami na changarawe.
Dkt. Samia ameyasema hayo leo Oktoba 7, 2025, katika eneo la Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza kumlaki na kumsikiliza ikiwa ni siku yake ya kwanza ya kampeni mkoani Mwanza.
Dkt. Samia amesema kuongozea bajeti katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kunalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za usafiri na kukuza maendeleo ya kiuchumi.
Pia, Dkt. Samia amefafanua kuwa iwapo atachaguliwa kuongoza kwa miaka mitano ijayo, basi Serikali yake atakayoiongoza itatekeleza ujenzi wa barabara ya Mwanza City Centre–Buhongwa–Usagara, ambayo itakuwa na njia nne.
Aidha, amebainisha kuwa mchakato wa kumpata mkandarasi uko katika hatua za mwisho baada ya tenda kutangazwa.
Vilevile, Dkt. Samia amesema katika kipindi cha miaka 5 ijayo iwapo atapewa ridhaa ya kuchaguliwa na kuongoza Taifa, kupitia Serikali amepanga kutekeleza ujenzi wa barabara za Mwanza City Centre–Igoma–Kisesa pamoja na Mkuyuni–Maina–Muhangu–Igoma, ambazo tayari zimefanyiwa upembuzi yakinifu na maandalizi ya ujenzi yanaendelea.
Akieleza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, Dkt. Samia amesema Serikali imekamilisha ujenzi wa barabara ya Buhongwa–Igoma yenye urefu wa kilomita 14 kwa gharama ya shilingi bilioni 22.7, sambamba na madaraja ya Mkuyuni na Mabatini ambayo yamegharimu shilingi bilioni 11.2.
𝙆𝙖𝙣𝙙𝙖 𝙮𝙖 𝙕𝙞𝙬𝙖 𝙬𝙖𝙣𝙖 𝙠𝙞𝙡𝙖 𝙨𝙖𝙗𝙖𝙗𝙪 𝙮𝙖 𝙠𝙪𝙢𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙖 𝙎𝘼𝙈𝙄𝘼 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙤 𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙫𝙪💚💛
Comments