Mwenyekiti wa UWT Taifa ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) awaomba wananchi wa Jimbo la Kibamba Wilaya ya Ubungo kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la Uchaguzi Oktoba 29, 2025, na kumpigia kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo Kumheshimisha akiwa kama Mwanamke na kutoa mfano kwa mataifa mbalimbali duniani kwa kumpa nafasi ya kuwania uongozi, na ni mara ya kwanza kwa CCM kumsimamisha na kumuamini Mwanamke kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chatanda ameyasema hayo tarehe 04, Oktoba 2025, wakati akinadi ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Stop Over Kimara, Jimbo la Kibamba jijini DSM na kuwaombea kura za kishindo Dkt. Samia SuluhunHassan, kwa Nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM, Angella Kairuki Mgombea Ubunge jimbo la Kibamba pamoja na madiwani wa Kata kupitia CCM.
Comments