Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) na Mratibu wa Kampeni za CCM Jijini DSM Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) awaomba Wanawake kumchagua kwa kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumpigia kura ya ndiyo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29, Oktoba, 2025, ili aweze kushinda na kushika dola, kwa Kuwa Dkt. Samia anauwezo na anaweza kuliongoza Taifa hili kwa kipindi cha Miaka mitano ijayo kwa kuwahudumia Watanzania.
Chatanda ameyasema hayo leo tarehe 19 Oktoba, 2025, katika Kongamano lililowakutanisha Wanawake wa Makundi mbalimbali Wajasiriamali (Wafanyabiashara Wadogowadogo) kutoka Wilaya ya Konondoni jijini DSM, waliokuwa wakipewa Elimu ya Biashara na Ujasiriamali katika Ukumbi wa Kiramuu Mafunzo yaliyoandaliwa na UWT Wilaya ya Kinondoni.
Comments