PICHA mbalimbali za Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa katika mkutano wake wa hadhara wa kampeni uliofanyika kata ya Nalasi,Jimbo la Tunduru Kusini,mkoa wa Ruvuma, leo Oktoba 19,2025, katika mwendelezo wa mikutano yake ya hadhara ya kampeni nchi nzima kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.
Akiwa katika mkutano huo wa kampeni pamoja na kunadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-30 ,Dkt.Nchimbi aliwashukuru wananchi wa Tunduru kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wake huku akiwaomba kujitokeza kwa wingi ifikapo Octoba 29,2025 kuwapigia kura za kishindo Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) .
Katika hatua nyingine Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Tunduru Kusini,Mhandisi Fadhili Sandali CHILOMBE na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Ndugu Sikudhani Yassin CHIKAMBO pamoja na Madiwani
Comments