Jimbo la Musoma Vijijini: WALIOTIA NIA WANASHIRIKI KWENYE KAMPENI ZA KUKITAFUTIA USHINDI MKUBWA CHAMA CHETU (CCM)
Timu ya Kampeni ya CCM ya Jimbo la Musoma Vijijini inaendelea kufanya kampeni zake kwa ufanisi mkubwa wenye mpangilio mzuri.
Wajumbe wa Timu ya Kampeni ni:
(i) Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma Vijijini
(ii) Wagombea 8 wa Udiwani wa Viti Maalum vya CCM
(iii) Sekretariati ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini
(iv) Viongozi wa Chama (CCM) wa Kata na Matawi kila panapofanyika kampeni
(v) Wafanyakazi wa Ofisi ya Mbunge, Prof Sospeter Muhongo
USHIRIKI MZURI WA WALIOTIA NIA KWENYE NAFASI YA UBUNGE NA UDIWANI
(i) Kila mahali tunapofanya kampeni, Waliotia nia kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani wanashiriki kuwaombea kura Wagombea wa Chama chetu (CCM) - nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani
(ii) Waliotia nia kwenye nafasi ya Ubunge wanashiriki vizuri wakiwa bega kwa bega na Mgombea Ubunge, Prof Sospeter Muhongo
HAZINA KUBWA YA CCM
Waliotia nia kwenye nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ni HAZINA kubwa ya Chama chetu.
Hawa ndugu zetu ni wasomi wazuri wenye uzoefu muhimu kwa faida ya Taifa letu. Hao ni:
(1) Senior Lecturer Dr Benjamin Mbeba
Development Studies & Sociology
PhD, MA & BA
(2) Mwl Bernard Merumba
Education, management & business studies
MBA & B.Ed (com)
(3) Advocate Zakayo Majinge
Corporate & commercial laws
LLM & LLB
(4) Kennedy Chiguru
Urban & Regional planning
MSc & BSc
Jimbo la Musoma Vijijini linaendelea kutekeleza kwa ufanisi mkubwa wenye matokeo mazuri ya Ilani za Uchaguzi za CCM na Dira za Maendeleo ya Taifa letu ikiwemo Dira mpya ya 2025-2050
PICHA zilizoambatanishwa hapa:
Picha kwenye boti, tukielekea Kisiwani Rukuba. Watiania kwenye Ubunge walishiriki kwenda kupiga kampeni kwenye visiwa vitatu vya Rukuba, Iriga na Kagongo
Picha Kijijini Kinyang'erere, Kata Bugwema
Kutoka kulia kwa Prof Muhongo:
Dr Mbeba (mwenye kifimbo), Advocate Majinge, Mwl Merumba na Ndugu Chiguru
TUENDELEE KUSHAWISHI WANANCHI WAJITOKEZE KWA WINGI KWENDA KUPIGA KURA NA WAIPIGIE CCM KURA NYINGI ZA USHINDI MKUBWA
Timu ya Uchaguzi (CCM)
Jimbo la Musoma Vijijini
Sun, 19 Oct 2025
Comments