KABILA AHUKUMIWA KIFO

Mahakama ya kijeshi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, leo Septemba 30 imemuhukumu aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Joseph Kabila adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya uasi na makosa mengine kadhaa.

Mwendesha mashtaka wa Serikali aliiomba Mahakama itoe hukumu ya kifo dhidi yake baada ya Serikali kumtuhumu Kabila kwa kushirikiana na Rwanda pamoja na Waasi wa kundi la M23 kuteka Miji muhimu ya Mashariki mwa Congo kupitia mashambulizi ya ghafla na hadi sasa wanaendelea kuishikilia.

Kabila ambaye amekuwa akishtakiwa kwa njia ya kutohudhuria tangu Julai huku akiwa hajulikani alipo, alikabiliwa na mashtaka ya uhaini, kushiriki katika harakati za uasi, kula njama na kusaidia vitendo vya kigaidi japokuwa mwenyewe amekuwa akikana vikali tuhuma hizo.

Mnamo mwezi wa tano mwaka 2025 Seneti ya Congo ilipitisha uamuzi wa kuondoa kinga ya kisheria aliyokuwa akiifurahia Rais Mstaafu Joseph Kabila kitendo ambacho alikikosa vikali na kukielezea kama ni kitendo cha kidikteta.

Joseph Kabila alikuwa akiishi nje ya Nchi kwa hiari yake mwenyewe lakini aliripotiwa kurejea Mjini Goma mwezi wa nne mwaka 2025 ambapo Goma ni miongoni mwa Miji inayodhibitiwa na Waasi wa M23 ambapo kwa sasa haijulikani kama bado yupo Goma ama la.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

LEO NI LEO KAMPENI ZA DKT. SAMIA SONGWE

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM