Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, leo anafanya mkutano mkubwa wa kampeni mjini Bukoba, mkoani Kagera.
Dkt. Samia ambaye yupo kwenye muendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, Jana amefanya katika Wilaya za Muleba, Misenyi na Karagwe ambapo ameeleza miradi mbalimbali iliyotekelezwa wakati wa uongozi wake wa miaka minne na kutoa ahadi lukuki atakazozitekeleza endapo wananchi watampatia ridhaa ya kuongoza tena Nchi kwa kumchagua katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29.
Baadhi ahadi alizozitoa katika mikutano hiyo ni; ujenzi wa Uwanja wa Ndege mkubwa wa kisasa wa Kimataifa, kujenga kongani za viwanda vikiwemo vya kuongeza thamani ya mazao ya samaki kuinua zao la alovera, zao la kahawa, kununua boti za uvuvi zitakazotolewa mkopo kwa wavuvi.
Pia, atahakikisha anakamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya maji, elimu, umeme, barabara pamoja na kujenga miradi mingine mipya.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
Comments