Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye jana Oktoba Mosi Kampeni zake zimetinga Mkoa wa Arusha, leo anatarajia kufanya mkutano mkubwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Jana Oktoba Mosi, 2025 Dkt Samia alipiga hodi Mkoa wa Arusha kwa kufanya Kampeni Usa-River Wilaya ya Arumeru, baada kumaliza Mkoa Kilimanjaro katika Uwanja wa Mashujaa Moshi Mjini na Boma-ng'ombe.
Baada ya kufanya uzinduzi wa kampeni kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe ijini Dar es Salaam Agosti 28, 2025, leo Oktoba 2, 2025 ameingia mkoa huo ukiwa ni Mkoa wa 19 baada ya kufanikisha kwa kiwango kikubwa kampeni katika mikoa mingine 18.
Tanzania Bara ni; Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora, Kigoma, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na Kilimanjaro.
Tanzania Visiwani; Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kusini Pemba.
Bado mikoa ya; Dar es Salaam, Manyara, Rukwa, Katavi, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara, Kagera, Mwanza, Mkoa wa Mjini Magharibi na Mkoa wa Kaskazini Pemba
Akiwa katika mikutano hiyo, Dkt. Samia hujinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika mikoa hiyo, pia hutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Aidha, Dkt. Samia amekuwa akisisitiza kudumisha Muungano na kuendelea kulinda amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Pia amewatoa wananchi wasiwasi kwamba hakutokuwa na vurugu kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko imara, hivyo siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu wajitokeze kwa wingi tena bila hofu kwenda kupiga kura na kurejea salama majumbani.
Pamoja na kuelezea kwa undani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. Emmauel Nchimbi, hutumia fursa hiyo kujinadi yeye, wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203
Comments