Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye jana Kampeni zake zimeingia kwa kishindo Mkoa wa Kilimanjaro, leo anatarajia kufanya mkutano mkubwa mjini Moshi.
Jana Septemba 30,2025 Dkt Samia alipiga hodi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kufanya Kampeni katika Wilaya za Same na Mwanga, baada kumaliza Mkoa wa Tanga katika miji ya Korogwe na Mombo.
Akiwa mkoani Kilimanjaro atahitimisha Kampeni kwa kufanya mkutano Bomang'ombe Wilaya ya Hai na hatimaye kuingia Mkoa wa Arusha kwa kufanya mkutano Usariver wilayani Arumeru.
Comments