Na Richard Mwaikenda, Dodoma
ZAIDI ya watu milioni 14.62 wamejitokeza kwenye mikutano moja kwa moja, milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika mikutano ya kampeni 77 ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika katika mikoa 21 kanda mbalimbali za nchi.
Mikutano hiyo iliyofana imefanyika katika kanda za Magharibi, Pwani, Kusini, Nyanda za Juu Kusini, kati, Pemba na Unguja (Zanzibar), vilevile Kanda ya Kaskazini.
Tathmini na mwenendo huo wa kampeni za Dkt. Samia vimetolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa NEC White House Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma leo Oktoba 5, 2025.
"Mikutano yote hiyo ya kanda kwa kanda, mkoa hadi mkoa, mahudhurio yamekuwa makubwa, hali hiyo inaonesha jinsi mgombea wetu wa urais, Dkt Samia Suluhu Hassan, anavyokubalika na wananchi kwa mamilioni, wameweka imani kubwa kwake.," amesema Kihongosi na kuongeza kuwa...
..Imani ya wananchi kwa Dk Samia Suluhu Hassan, siyo bahati wala mkumbo, bali imechagizwa na uongozi wenye mafanikio makubwa katika miaka minne aliyoshika usukani wa urais."
Oktoba 7, 2025 kampeni za Dkt. Samia zinaanza kurindima katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kupiga hodi Mkoa wa Mwanza.
Comments