MAMBO YAMEIVA KAMPENI ZA DKT.SAMIA MULEBA

BASHASHA, NDEREMO vikiwa vimetawala Mjini Muleba Kagera,katika mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) .Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 15, 2025. 









 ‎Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 15 anatinga Mkoa wa Kagera baada ya  juzi Oktoba 13,2025 kufanya  Kampeni zake katika mkutano mikubwa kwenye Uwanja Bombambili, Chato na KATORO mkoani Geit. 

‎Anaingia Mkoa huo leo  kwa kuanza kampeni Muleba, Misenyi na baadaye mchana katika Jimbo la  Karagwe linalogombewa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa.

‎Baada ya kufanya uzinduzi wa kampeni kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe ijini Dar es Salaam Agosti 28, 2025, leo Oktoba 15, 2025 Dkt. Samia ameingia mkoa huo ukiwa ni Mkoa wa 26  baada ya kufanikisha kwa kiwango kikubwa kampeni katika mikoa mingine 25.

‎Tanzania Bara ni;  Morogoro, Dodoma, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Singida, Tabora, Kigoma, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha, Manyara, Mwanza, Mara, Simiyu,  Shinyanga na Geita.

‎Tanzania Visiwani; Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kusini Pemba.

‎Bado mikoa ya; Dar es Salaam,  Rukwa, Katavi, Mkoa wa Mjini Magharibi na Mkoa wa Kaskazini Pemba

‎Akiwa katika mikutano hiyo, Dkt. Samia hujinadi kwa kuelezea mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika  mikoa hiyo, pia hutoa ahadi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa miaka mingine mitano endapo atashinda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29.

‎Aidha, Dkt. Samia amekuwa akisisitiza kudumisha Muungano na kuendelea kulinda amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

‎Pia amewatoa wananchi wasiwasi kwamba hakutokuwa na vurugu  kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko imara, hivyo siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu  wajitokeze kwa wingi tena bila hofu kwenda kupiga kura na kurejea salama majumbani.

‎Pamoja na kuelezea kwa undani Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Dkt. Samia ambaye mgombea wake mwenza ni Dkt. Emmauel Nchimbi, hutumia fursa hiyo kujinadi yeye,  wagombea ubunge na madiwani wa chama hicho.


‎IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA