MASWA KUMEPAMBAZUKA KAMPENI ZA DKT. SAMIA

Wasanii wa wilayani Maswa wakionesha ishara ya miaka mitano tena ya kumtakia ushindi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan walipokuwa wakimsubiri azungumze na wananchi na kuwaomba kura leo Oktoba 11,2025 akitokea Bariadi.


Mapema kabisa asubuhi hii tayari maelfu ya wananchi wa Maswa mkoani Simiyu wamejitokeza pembezoni mwa barabara kwa kazi kubwa moja ya kumuhakikishia Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 kura za uhakika na kupelekea kupata ushindi wa kishindo siku ya Oktoba 29.

Moja kati ya jambo kubwa na lililogusa mioyo ya wananchi hawa wa Maswa ni pale ambapo Dkt. Samia alipoamua kuchochea thamani ya zao la Pamba wilayani humo na nchi nzima kwa ujumla.

Dkt. Samia kupitia Serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka 4 iliyopita akiwa amekalia kiti cha Urais, ameweza kukuza sekta ya viwanda kwa kuwahimiza wawekezaji kutumia malighafi za ndani, hususan zao la pamba, katika kuongeza thamani ya mazao na kuleta ajira kwa wananchi jambo ambalo limewagusa moja kwa moja wananchi wa Maswa hapa mkoani Simiyu.

Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM ambapo siku ya leo Dkt. Samia anaagana na wananchi wa Simiyu na kuendelea na ratiba yake ndani ya mkoa wa Shinyanga.










 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM

DKT. SAMIA AWASILI ZANZIBAR

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA