DKT. SAMIA AAHIDI KULIPA FIDIA KWA WALIOPISHA UJENZI WA BARABARA YA SITALIKE - KIBAONI

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, DKT. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwalipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa barabara ya Sitalike- Kibaoni mkoani Katavi.


Amesema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu, ataiagiza Wizara ya ujenzi kufanya upembuzi wa majina ya wanaostahili ili walipwe stahiki zao.


Ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 18, 2025 alipokuwa akijinadi katika mkutano mkubwa wa Kampeni kwenye viwanja vya Azimio Mjini Mpanda mkoani Katavi ikiwa ni siku ya 52 tangu aanze Kampeni Agosti 28, 2025.


Aidha, Dkt. Samia amesema kuwa watahakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango Cha lami yenye urefu wa Km. 74 ambayo kwa hivi sasa inajengwa Km 50 na baadaye itamaliziwa Km. 24.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA