Alhamisi, 09 Okt 2025, Mgombea Urais wa CCM, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan alifanya kampeni zenye mafanikio makubwa sana kwenye Kiwanja cha Karume cha Musoma Mjini.
Wagombea Ubunge wa CCM wa majimbo ya Musoma Mjini (Mhe Mgore Kigera), Tarime Mjini (Mhe Esther Matiko), Tarime Vijijini (Mhe Mwita Waitara), Rorya (Mhe Jafari Chege), na Musoma Vijijini (Mhe Prof Muhongo), walipata fursa za kuomba kura za wagombea wote wa CCM, yaani kura za Mgombea Urais, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kura za Wabunge wa majimbo na kura za Wadiwani wote.
Wagombea Ubunge Viti Maalum wa Mkoa wa Mara (Mhe Agnes Marwa & Ghati Chomete) nao waliomba, kwa mafanikio makubwa, kura za CCM kama ilivyoelezwa hapo juu.
CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa inatupatia mchango wa Prof Sospeter Muhongo kwenye kampeni za jana za Musoma Mjini - tafadhali msikilize.
Timu ya Kampeni
Jimbo la Musoma Vijijini
Ijumaa, 10 Okt 2025
Comments