.Na Richard Mwaikenda, Buhongwa, MWANZA
Mkoa wa Mwanza wameahidi kumpatia ushindi wa kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika majimbo yote 9 ya Uchaguzi.
Ahadi hiyo imetolewa kwa niaba ya wananchi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Michael Nasanja alipokuwa akitoa salamu za Mkoa akimkaribisha DKT. Samia mkoani humo katika mkutano wa Kampeni katika Kata ya Buhongwa, Nyamagana Oktoba 7, 2925.
Amesema kuwa wananchi watampatia ushindi huo kutokana na kuuletea Mkoa huo maendeleo makubwa yanayoonekana na kila mtu.
Serikali inayoongozwa na Rais, DKT. Samia imepeleka mkoani humo zaidi ya sh. 5 za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara, afya, elimu, maji, Kilimo, nishati na mawasiliano.
Comments