Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amewahakikishia Watanzania hali ya Amani, Utulivu na Usalama siku ya tarehe 29 Oktoba 2025 katika zoezi la kupiga kura nchi nzima.
Pamoja na hilo, Dkt. Samia ametoa onyo kali kwa mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kuvuruga amani ya Tanzania.
"..𝘯𝘢 𝘩𝘢𝘱𝘢 𝘯𝘪𝘴𝘦𝘮𝘦 𝘯𝘥𝘶𝘨𝘶 𝘻𝘢𝘯𝘨𝘶 𝘩𝘪𝘭𝘪 𝘯𝘪𝘸𝘢𝘵𝘰𝘦 𝘩𝘰𝘧𝘶, 𝘬𝘶𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘶 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘵𝘪𝘴𝘩𝘢𝘵𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘪𝘭𝘪 𝘬𝘶𝘸𝘢𝘧𝘢𝘯𝘺𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘶 𝘸𝘢𝘴𝘪𝘵𝘰𝘬𝘦 𝘵𝘢𝘳𝘦𝘩𝘦 29 𝘬𝘸𝘦𝘯𝘥𝘢 𝘬𝘶𝘱𝘪𝘨𝘢 𝘬𝘶𝘳𝘢,.."
"..𝘯𝘪𝘯𝘢𝘺𝘦𝘻𝘶𝘯𝘨𝘶𝘮𝘻𝘢 𝘩𝘢𝘱𝘢 𝘯𝘪 𝘈𝘮𝘪𝘳𝘪 𝘑𝘦𝘴𝘩𝘪 𝘔𝘬𝘶𝘶 𝘸𝘢 𝘯𝘤𝘩𝘪 𝘩𝘪𝘪, 𝘯𝘢𝘸𝘢𝘢𝘮𝘣𝘪𝘢 𝘸𝘢𝘴𝘪𝘵𝘩𝘶𝘣𝘶𝘵𝘶, 𝘬𝘪𝘣𝘢𝘵𝘪 𝘵𝘶 𝘬𝘪𝘬𝘪𝘱𝘢𝘴𝘶𝘬𝘢 𝘴𝘪𝘴𝘪 𝘵𝘶𝘬𝘰 𝘯𝘢𝘰, 𝘵𝘶𝘮𝘦𝘫𝘪𝘱𝘢𝘯𝘨𝘢 𝘷𝘪𝘻𝘶𝘳𝘪..𝘵𝘰𝘬𝘦𝘯𝘪 𝘮𝘬𝘢𝘱𝘪𝘨𝘦 𝘬𝘶𝘳𝘢 𝘬𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘳𝘶𝘥𝘪𝘯𝘪 𝘯𝘺𝘶𝘮𝘣𝘢𝘯𝘪 𝘮𝘬𝘢𝘱𝘶𝘮𝘻𝘪𝘬𝘦, 𝘩𝘢𝘬𝘶𝘯𝘢 𝘩𝘰𝘧𝘶 𝘯𝘢 𝘩𝘢𝘬𝘶𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘰𝘨𝘰𝘱𝘢, 𝘵𝘰𝘬𝘦𝘯𝘪 𝘮𝘬𝘢𝘱𝘪𝘨𝘦 𝘬𝘶𝘳𝘢"
Aidha, Dkt. Samia amesema CCM imedhamiria kuendelea kufanya kazi na kueleza kuwa miaka 5 iliyopita kazi imefanyika na kuelekea mitano mingine CCM inajiamini kuendelea kutekeleza kwa kishindo ilani yake yenye kugusa matakwa ya Watanzania katika kuleta maendeleo endelevu na kuinua Utu hivyo kuna kila sababu ya Watanzania kuendelea kukiamini na kumchagua yeye katika nafasi ya Urais wa Tanzania, kuwachagua Wabunge na Madiwani wote wanaotokana na CCM ili kukamilisha mafiga matatu.
Dkt. Samia amekamilisha ratiba ya mikutano yake ya kampeni leo tarehe 10 Oktoba 2025 ndani ya mkoa huu wa Simiyu mara baada ya kumaliza mkoani Mara na kuanzia kesho tarehe 11 Oktoba 2025 anatarajiwa kuendelea katika mkoa wa Shinyanga.
Comments