WENJE ASHANGAA TAKWIMU ZA MIRADI YA MAENDELEO ZINAZOSHUSHWA KATIKA KAMPENI ZA DKT. SAMIA


 Ezekia Wenje ambaye ambaye hivi karibuni amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama Cha Demokrasia  na Maendeleo (CHADEMA), ameshangazwa jinsi takwimu za kweli za miradi ya maendeleo zinazoshushwa na wagombea kwenye mikutano ya kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, DKT. Samia Suluhu Hassan.


‎Ameonesha mshangao huo alipokaribishwa kutoa salamu katika mkutano wa kampeni za CCM katika MJi wa Kayanga wilayani Karagwe, Kagera leo Oktoba 15,2025.


‎"Mheshimiwa Mwenyekiti na Mgombea wa CCM nimekaa na nyie siku tatu nimegundus kuwa usichokijua ni sawa na usiku wa giza," amesema Wenje na kuongeza...


 ...CCM hoyee, waheshimiwa wananchi wenzangu nimekaa ndani ya CCM siku tatu nimesikiliza, nimetafakari kila sehemu tulipoenda nasikiliza hizo takwimu nabaki nashangaa, nikagundua kumbe sisi kule bomani, tunapekua taatifa ndogondogo kwenye mitandao za kuichafua Serikali bila kujua takwimu za kweli. Ni sawa na usiku wa giza."


"Ndugu Mgombea kelele hizo ndogo ndogo zisikutishe haziwezi kukuzuia kuingia Ikulu, hata kwa Mungu shetani alileta kelele akafukuzwa, utashinda kwa kishindo," amesisitiza Wenje.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

DKT.NCHIMBI ATUA RASMI SONGEA KUSAKA KURA ZA CCM

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA