WENJE ATISHIA KUWATAJA WANAOIFADHILI CHADEMA KUTOKA NJE

 


Na Richard Mwaikenda, Rukwa

Ezekia Wenje ambaye hivi karibuni amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ametishia  kuwataja watu walio Nje ya Nchi Wanaoifadhili CHADEMA kwa lengo la kusababidha vurugu nchini.


Ametoa kauli hiyo alipopewa wasaa wa kutoa salamu katika mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Kizwite Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa Oktoba 19, 2025.


"Leo CHADEMA imegeuka kuwa NGo's inapewa  fedha na wanaharakati walioko Nje ya Nchi, wanachangiwa kwenye mitandao, yaani Chama kiko Tanzania lakini kinaendeshwa kwa 'remote control'na watu walio nje wenye fedha zao. na wakileta pambano nitakuja na orodha ya majina yao,"amesema Wenje.


"CCM hoyee, kwa hiyo mimi kwa maoni yangu na dhamira yangu naamini nimechagua njia iliyo sahihi. Naamini Watanzania tutakuwa salama na tutakuwa tumechagua njia sahihi Oktoba 29 tukimpigia Dkt Samia kura, wabunge wa CCM na Madiwani wa CCM."


Jana Oktoba 18, 2025, Wenje akiwa katika mkutano wa Kampeni Mpanda Mjini, mkoani Katavi  alitaja baadhi ya nchi za nje zinazofadhili kuwa ni; Marekani, Norwey, Uingereza na Kenya.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA