Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 24, 2025 amekagua miundombinu ya usafiri wa mwendo kasi pamoja na mali nyingine ikiwemo nyingine zilivyoharibiwa kutokana na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 jijini Dar es Salaam.
Maeneo yaliyokaguliwa ni pamoja na Kituo cha Mafuta cha Puma ilichopo kimara baruti, vituo vya mwendo kasi vya Kimara Korogwe na Kimara Mwisho pamoja na kituo cha Mafuta cha Rupees kilochopo Kimara Stop Over.
Kadhalika, Mheshimiwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu ametoa rai kwa Watanzania kuilinda Tanzania na kufahamu kwamba miundombinu iliyopo nchini ni mali ya umma, na inajengwa kwa fedha za Watanzania.








Comments