๐—–๐—–๐—  ๐—›๐—”๐—œ๐—ง๐—”๐—ฆ๐—œ๐—ง๐—” ๐—ž๐—จ๐—ช๐—”๐—–๐—›๐—จ๐—ž๐—จ๐—Ÿ๐—œ๐—” ๐—›๐—”๐—ง๐—จ๐—” ๐—ช๐—”๐—ง๐—จ๐— ๐—œ๐—ฆ๐—›๐—œ ๐—ช๐—” ๐—จ๐— ๐— ๐—” ๐—ช๐—”๐—•๐—”๐—•๐—”๐—œ๐—ฆ๐—›๐—”๐—๐—œ - ๐— ๐—ช๐—˜๐—ก๐—˜๐—ญ๐—œ ๐—ž๐—˜๐—ก๐—”๐—ก๐—œ

๐˜ผ๐™จ๐™š๐™ข๐™– ๐˜พ๐˜พ๐™ˆ ๐™ž๐™ฃ๐™– ๐™ฌ๐™–๐™Ÿ๐™ž๐™—๐™ช ๐™ฌ๐™– ๐™ ๐™ช๐™›๐™ช๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ก๐™ž๐™– ๐™ช๐™ฉ๐™š๐™ ๐™š๐™ก๐™š๐™ฏ๐™–๐™Ÿ๐™ž ๐™ฌ๐™– ๐™ž๐™ก๐™–๐™ฃ๐™ž ๐™ฎ๐™–๐™ ๐™š ๐™ ๐™ฌ๐™–๐™ ๐™ช๐™ฌ๐™– ๐™จ๐™š๐™ง๐™ž๐™ ๐™–๐™ก๐™ž ๐™ž๐™ฃ๐™–๐™ฉ๐™ค๐™ ๐™–๐™ฃ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™˜๐™๐™–๐™ข๐™– ๐™๐™ž๐™˜๐™๐™ค.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ž๐—ถ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜€๐—ถ amewataka watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwa kutanguliza utu na muda.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama na jumuiya wa mkoa wa Dar es salaam, Mwenezi Kenani amesema kuwa wapo baadhi ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakilalamika kuwa kwanini viongozi wa chama wamekuwa wakifuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo ameeleza kuwa kitendo hicho ni kudhiirisha kuwa watumishi hao hawapo tayari kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu na kusema kufanya hivyo ni kuikosea heshima serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na CCM na kuongozwa na Mwenyekiti na Rais Mhe. Dkt. ๐—ฆ๐—ฎ๐—บ๐—ถ๐—ฎ ๐—ฆ๐˜‚๐—น๐˜‚๐—ต๐˜‚ ๐—›๐—ฎ๐˜€๐˜€๐—ฎ๐—ป.

Mwenezi Kenani ametuma ujumbe kwa baadhi ya watumishi hao akisema kuwa CCM hiataacha kufuatilia kila hatua katika utoaji hudumu wao kwa wananchi na utekelezaji wa miradi kwakuwa inayotekelezwa ni ilani ya uchaguzi ya CCM waliyoinadi.

"kuna baadhi ya watumishi wa umma wanasema chama kinawafatafata, waambieni tuna wajibu wa kuwafata kwakuwa ilani inayotekelezwa ni yetu na tutawafata kila wakati kuhakikisha wanafanya kazi iliyokusudiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia"

"Ikiletwa fedha ya kituo cha afya basi chama kitakuja kukagua matumizi sahihi ya fedha hizo, hatutaacha kufanya hivyo kwakuwa watumishi wazembe ndiyi wenye kusababisha CCM ionekane haifanyi kazi"



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€