DKT. KIKWETE AKUTANA NA RAIS MUTHARIKA

Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) (Panel of Elders, POE) akiwa katika picha ya pamoja na Profesa Arthur Peter Mutharika, Rais wa Malawi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya  Jumuiya ya SADC, baada ya kufanya naye mazungumzo jana Ijumaa jijini Lilongwe, Malawi. 


Pamoja nao ni Mama Joyce Banda, Rais Mstaafu wa Malawi, ambaye ni Mjumbe wa Jopo hilo la Wazee. Katika mazungumzo yao, pamoja na mambo mengine, Viongozi hao walipata fursa ya kumweleza Rais Mutharika kuhusu kazi zilizofanywa na zinazoeandelea kufanywa na POE katika kusuluhisha migogoro katika nchi za Ufalme wa Lesotho, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi na kwa sasa Madagascar. 

Kimuundo, POE ni moja ya vyombo vya kuzuia migogoro na kurejesha amani katika nchi za SADC ambacho kinaripoti moja kwa moja kwenye Asasi ya SADC Troika, ambayo nchi ya Malawi ndiyo Mwenyekiti wake kwa sasa.






 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

Wasifu wa Kizza Besigye

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026