DKT. MIGIRO AONGOZA KIKAO BODI YA WADHAMINI SHULE YA UONGOZI MWALIMU NYERERE

Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, kwenye Kikao cha Bodi ya Wadhamini wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), kilichoketi leo tarehe 4 Machi 2026, Kibaha, mkoani Pwani. 

Wajumbe wengine waliohudhuria kikao hicho ni; Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Chakil Felizardo Passadas Aboobacar, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU-PF (Zimbabwe), Jacob Francis Nzwindamilimo Mudenda, Chama cha SWAPO (Namibia), kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dkt. Samuel Abraham Peyavali Mushelenga na Chama cha MPLA (Angola) kimewakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Frederico Toth Jorge De Miranda.






Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na  Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Fikile Mbalula (kulia pichani) pia Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Chakil Felizardo Passadas Aboobacar (kushoto pichani), kabla ya kuanza Kikao cha Bodi ya Wadhamini wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), kilichoketi leo tarehe 4 Machi 2026, Kibaha, mkoani Pwani. Wajumbe wa kikao hicho ni Makatibu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Vyama vingine ni SWAPO (Namibia), ZANU - PF (Zimbabwe) na MPLA (Angola).


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

NI MAKOSA WANAFUNZI KUFIKA SHULE SAA 1:15 ASUBUHI

MAFAO YA MAKAMU WA RAIS ALIYEJIUZULU

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR