Ni nadra sana kusikia watoto wa Viongozi wakuu wa nchi hasa Rais hawajulikani, lakini Wakati wa Utawala wa Dkt John Magufuli Hilo liliwezekana aliiweka mbali sana familia yake na serikali, vyombo vya Habari na hata masikioni mwa watu. Katika kipindi chote Cha utawala wa Rais wa awamu ya Tano Dkt Magufuli, wengi walikosa kujua mengi kuhusu familia yake, jambo lililowafanya kuwa na faragha sana. Hata hivyo, kwenye mazishi ya kitaifa jijini Dodoma,2021 siri hizi zilifichuka. kwenye mazishi ya kitaifa jijini Dodoma, familia yake ilijulikana kuwa Dkt Magufuli ameacha watoto saba na wajukuu 10. Waziri Profesa Palamagamba Kabudi ambaye ndiye Alisoma wasifu huo wa JPM Alitaja watoto hao ni Suzzan John Magufuli, Edna John Magufuli, Joseph John Magufuli (pichani), Jesca John Magufuli, Ruth John Magufuli, Jurgen John Magufuli, Jeremiah John Magufuli na Juliana John Magufuli aliyefariki dunia wakati baba yake akiwa waziri. Jina maarufu kwa Watanzania mpaka Leo na wengi walimfahamu mwanaye tan...
Comments