Watu wengi wanafikiri utajiri ni bahati. Wengine wanafikiri ni kurithi. Lakini ukweli ni huu: Utajiri ni vita ya kisaikolojia ambapo silaha pekee ni kafara. Usidanganywe na picha za Instagram za watu wakiwa kwenye fukwe; hapo ni mwisho wa safari. Leo nataka nikuchane kuhusu mwanzo wa safari ule upande wa giza, jasho, na damu ambao haupigwi picha.
Umesema unatamani kuwa tajiri? Swali siyo "unatamani kiasi gani", swali ni "upo tayari kupoteza nini?"
1. KAFARA YA USINGIZI: "THE MIDNIGHT ASSASSIN"
Wakati dunia imetulia saa nane za usiku, hapo ndipo hatima za watu zinapoandikwa. Maskini hutumia masaa hayo kuota ndoto, lakini tajiri hutumia masaa hayo kuzitengeneza ndoto.
Gharama: Macho mekundu, uchovu wa akili, na mwili unaolalamika.
Ukweli: Huwezi kuwa tajiri kwa kufanya kazi masaa nane (8) kama kila mtu mwingine. Lazima uibe masaa ya ziada kutoka kwenye usingizi wako. Unapokuwa macho wakati wenzako wamelala, unajipa nafasi ya kuwa mbele yao kwa hatua elfu moja. Usingizi ni anasa ambayo huna sifa ya kuipata mpaka akaunti yako itakapokuwa inazalisha pesa ukiwa umelala.
2. KAFARA YA MAHUSIANO SUMU (THE SOCIAL SURGERY)
Hii ndiyo kafara inayoumiza zaidi. Utajiri unahitaji "upasuaji" wa marafiki.
Huwezi kukimbia marathon ukiwa umebeba magunia ya mchanga mgongoni. Marafiki wanaopenda starehe, wanaolalamika kuhusu serikali kila siku, na wanaotumia wikendi nzima kunywa pombe hao ndio magunia yako.
Gharama: Utaitwa msaliti. Utaitwa una dharau. Utaitwa "umejificha".
Ukweli: Lazima ukubali kuwa mpweke. Siri ya matajiri ni kwamba walikubali kutembea peke yao kwenye jangwa la utafutaji ili waje kukutana na matajiri wenzao kwenye kilele cha mlima. Kama marafiki zako watano ni maskini, wewe ni wa sita.
3. KAFARA YA EGO NA MUONEKANO (INCOGNITO MODE)
Dhambi kubwa ya maskini ni kutaka kuonekana tajiri kabla ya kuwa tajiri.
Unanunua simu ya milioni tatu kwa mkopo, wakati huna hata kiwanja. Unanunua nguo za gharama ili upate sifa mtaani, wakati biashara yako haina mtaji.
Kafara: Lazima uwe tayari kuonekana "fukara" wakati unajenga himaya. Vaa nguo zilezile, piga miguu (tembea) au panda daladala, huku faida yako yote ukiirudisha sokoni.
Siri: Utajiri wa kweli haupigi kelele. Kelele hupigwa na "Matusi ya Rehani".
4. KAFARA YA BURUDANI (THE KNOWLEDGE WAR)
Ubongo wako ni injini. Ukilisha vichekesho vya TikTok na tamthilia za kila siku, utazalisha maisha ya kichekesho.
Matajiri wanatoa kafara ya burudani kwa ajili ya elimu ya fedha. Badala ya "Playlist" ya nyimbo za mapenzi, sikiliza namna ya kuwekeza kwenye hisa. Badala ya kuangalia mpira saa nne, soma kitabu cha mauzo (Sales) kwa saa nne.
Gharama: Utasikia kichwa kinauma kwa kufikiri. Hivyo ndivyo misuli ya utajiri inavyokua. Umaskini ni rahisi kwa sababu hauhitaji kufikiri, utajiri ni mgumu kwa sababu unadai akili yako yote.
5. KAFARA YA AMANI YA MOYO (THE HIGH STAKES)
Utajiri siyo kwa ajili ya watu wenye mioyo myepesi. Ni kafara ya amani yako.
Kutakuwa na siku ambazo utaweka kila kitu ulichonacho kwenye mradi mmoja, na huna uhakika kama utarudi. Hapo ndipo "ujasiri wa kishujaa" unapotakiwa.
Gharama: Kukosa hamu ya kula, hofu ya kufilisika, na shinikizo la moyo.
Ukweli: Bila riski, hakuna utajiri. Lazima uwe tayari kupoteza kila kitu ili upate kila kitu.
JE, UPO TAYARI KULIPIA?
Utajiri una siri moja kuu: Haupendi wazembe. Ulimwengu hautupi kile tunachohitaji, unatupa kile tunachostahili baada ya kulipia gharama.
Kama upo macho sasa hivi unasoma hii makala, tayari umeanza kutoa kafara ya muda wako. Lakini usishie hapa. Nenda kafanye kazi mpaka dunia ijue jina lako. Wenzio walale, wewe pambana. Wenzio wacheke, wewe wekeza. Wenzio wale bata, wewe kula jasho lako.
Mwisho wa siku, hakuna kitu kinachouma kama majuto ya kusema "Ningejua ningepambana."
#MatajiriWatarajiwa #KafaraYaMafanikio #Pambana #Mindset #SuccessQuotes #TanzaniaFinance #HustleStrategy

Comments