TPDC YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU BEI YA MAFUTA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ndg, Mussa Mohammed Makame amesema Watanzania hawapaswi kuwa na hofu kwani mpaka sasa nchi haijapata athari yoyote.

Ameyasema hayo jijini Dodoma leo Machi 11, 2026 alipokuwa akijibu swali la mwandishi kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta kufuatia vurugu zinazoendelea katika baadhi ya maeneo duniani katika mkutano wa kuelezea mafanikio ya TPDC katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kauli hiyo inaenda sambamba na ufafanuzi uliotolewa hivi karibuni na Waziri wa Nishati, Deogratias Ndejembi, aliyewahakikishia wananchi kuwa hali ya upatikanaji wa mafuta nchini iko salama.

Ameeleza kuwa mfumo wa uagizaji wa mafuta nchini hupangwa mapema, ambapo mafuta yanayotumika kwa mwezi fulani huagizwa takribani miezi miwili kabla.
Kwa mfano, mafuta yanayotumika mwezi Machi yaliagizwa mwezi Januari, na yatakayotumika Aprili yaliagizwa Februari.












 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025