MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imewezesha kusajiliwa kwa Kampuni 16 za kitanzania kuuza matunda ya parachichi nchini China.
Mafanikio hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Prof. Joseph Ndunguru wakati akielezea mafanikio ya TPHPA wakati wa Serikali ya Awamu 6 inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mkutano na vyombo vya Habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jijini Dodoma Machi 24, 2026.

Comments