Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Khadija Ngasongwa, akielezea namna tume hiyo inavyoshirikiana na taasisi zingine kufanya uchunguzi kubaini sababu za mabando ya simu kuisha mapema kabla ya muda.
Khadija ameyasema hayo alipokuwa akielezea mafanikio ya Tume hiyo kuhusu miradi ya maendeleo na fursa kwa vijana katika Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, leo Machi 05, 2026, katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

Comments