WILLIAM LUKUVI AFARIKI DUNIA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi (70) amefariki dunia saa 1:00 asubuhi ya leo Jumatano, Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Kifo hicho kimetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka juu ya msiba huo wa Lukuvi aliyezaliwa Agosti 15, 1955.

Taarifa hiyo imeeleza Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isiman, Mkoa wa Iringa amefariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

“Rais anatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo,” amesema Dk Kusiluka.

Lukuvi alikuwa miongoni mwa wabunge waandamizi bungeni ambaye amekuwa mbunge wa Ismani kuanzia mwaka 1995 hadi sasa akihudumu kwa zaidi ya miaka 30.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

Wasifu wa Kizza Besigye

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

MATUKIO RAIS, AMIRI JESHI MKUU DKT. SAMIA AKIZINDUA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA (MMUT)