Leo tarehe 14/04/2026 nimepata fursa ya kuwa Mgeni Maalum katika uzinduzi wa programu ya IMBEJU jijini Dodoma.
Chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais, Dr Samia Suluhu Hassan, Tanzania inaendelea kushuhudia viongozi wachapakazi, wenye maono na wanaosimamia kwa vitendo maendeleo ya wananchi.
Mfano mzuri ni Mheshimiwa Dr Neema Peter Majule, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, ambaye ameandika historia kwa kuwezesha kina mama kupata mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.13 kupitia programu ya IMBEJU chini ya CRDB Bank Foundation.
Nimepata pia fursa ya kukutana na Mkurugenzi wa CRDB Foundation, Tully Esther Mwambapa, ambapo tumebadilishana mawazo kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kunufaisha wanawake wa Mkoa wa Kagera. Ni matarajio yangu kuwa fursa hizi zitafika Kagera, hivyo ni muhimu tujiandae kuzipokea na kuzitumia kikamilifu.
Aidha, ninaipongeza CRDB Bank chini ya uongozi wa Abdulmajid Nsekela kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuinua uchumi wa Mtanzania.
Ninawahimiza kina mama wote kutumia mikopo hii kwa nidhamu na kuzingatia mafunzo waliyopewa kupitia programu ya IMBEJU, ili kujenga biashara imara na maisha bora zaidi.
#IMBEJU #UwezeshajiWanawake #CRDB #Maendeleo #KaziInaendelea
Comments