Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge amefanya uzinduzi wa kuchimba visima ikiwa kisima kimoja kitaghalimu Sh. milioni 12 mpaka kukamilika kwake na vitachimbwa katika Jimbo la Mbeya Mjini ambapo kazi hiyo imeanza Kata ya Itende iliyopo Wilaya ya Mbeya, Mkoa wa Mbeya kwa lengo la kupunguza kero ya maji kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Itende Kati, Metson Shongwe amemshukuru Mbunge kwa kuwaona na kuwachimbia kisima katika mtaa wao uliyopo katika kata ya Itende.
Naye chifu wa eneo hilo, Juma Jojo amesema nikweli idadi ya watu imeongezeka na kupelekea huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kuwa haba kwa hiyo kupitia kisima kinacho chimbwa kitasaidia kutatua kero hiyo.
Diwani wa kata ya Itende, Andambike Mwakyusa amesema wakati wa kampeni waliwasilisha kipaumbele chao cha uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa Mbunge Mwalunenge na leo ameitatua ikiwa hata miezi minne bado haijakwisha tangu aampe bungeni.

Comments