WALIOFUKUA KABURI LA KIYEUYEU IRINGA WAILILIA TANRODS


SIKU chache baada ya kung’olewa kwa kaburi la kihistoria la Martine Kiyeyeu na mengine 21 ya ukoo huo, Kitongoji cha Isimila, Kijiji cha Ugwachanya, wilayani Iringa, vijana 31 waliofanya kazi hiyo wamelalamikiwa kutolipwa fedha zao walizoahidiwa.
Zoezi la kuondoa makaburi hayo ambalo limeshangaza wengi kutokana na imani ya kutohamishika iliyokuwa imetawala, lilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita bila madhara yoyote.
Wakizungumza na Mwananchi jana, vijana hao walidai kuwa makubaliano baina yao na Wakala wa barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Iringa, ni kulipwa Sh1,420,000 baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhamisha makaburi yote 22 ya ukoo huo.
Akizungumza kwa niaba wenzake, Litus John, ambao Mwananchi ilikuta wakiwa wamejikusanya kijiji jirani cha Wenda, alisema licha ya kazi ngumu waliyofanya, hawajakabidhiwa fedha zao.
“Tunashangaa kwanini hawajatulipa fedha yetu licha ya kazi ngumu na hatari tuliyofanya, haya makaburi yalitakiwa kuhamishwa na wananchi wa Kijiji cha Ugwachanya, lakini historia ya kaburi la Kiyeyeu iliwaogopesha, hivyo kati ya 31 waliohamisha ni wawili tu waliotoka Ugwachanya,” alisema John.
Alisema makubaliano katika vikao walivyofanya, ilikuwa wapatiwe fedha hiyo siku ya pili ya zoezi la kuhamisha mabaki ya marehemu wa familia ya Kiyeyeu, fedha ambayo hawajapatiwa.
Kijana mwingine, Brown Duma, alisema jana asubuhi walimfuata mwenyekiti wa zoezi la kuhamisha makaburi hayo,  kujua hatma ya malipo yao, lakini hawakufanikiwa kumuona jambo linalowapa wasiwasi.
“Kibaya zaidi hawajaja hata kutushukuru, zoezi lile lilikuwa gumu kuliko watu wanavyodhani, tulijitoa muhanga kwa sababu tunahitaji maendeleo ya kijiji chatu, tunashuhudia wakija kuangalia na kugeuza bila kutwambia lolote,” alisema Duma.
Duma alisema iwapo leo hawatalipwa, wataandamana hadi ofisi za Tanroads kujua hatma yao, baada ya kukamilisha zoezi gumu lililoogopesha wengi.
Wakisumulia jinsi walivyojisikia wakati wakianza zoezi hilo, walisema waliogopa lakini baadaye wakajitoa mhanga na kuchimba hadi walipokutana na fuvu la kichjwa la Martine Kiyeyeu, ambaye anasadikiwa kuzikwa kati ya miaka 40 na 50 iliyopita.
“Sio kazi ndogo ile, tulijitahidi kwa kweli na tunashangaa hata asante hatujapewa japo tulijitosa, tulikuwa tayari kwa lolote, tukiamini tutaongeza fedha,” alisema.
Walisema waliamua kufanya ili kuongeza kipato na kwamba, waliami kuhamishwa kwa makaburi hayo ambayo yalisababisha umeme kuhamishiwa upande wa pili kabla ya kuendelea kwenye njia yake, kutasaidia kuharakisha maendeleo ya kijiji chao.
Hata hivyo, juhudi za kumpata mwenyekiti wa zoezi hilo hazikufanikiwa. Makaburi hayo yamehamishwa kupisha upanuzi wa  barabara ya Tanzam kutoka eneo la Kitwiru hadi Mafinga.
Meneja wa Tanroads mkoani Iringa, Paul Lyakulwa, alisema kutokana na mazungumzo yao na ukoo wa Kiyeyeu, ilionyesha hakuna ugumu wa kuhamisha makaburi hayo. 
HABARI KWA HISANI YA TOVUTI YA MWANANCHI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA