HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI
MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA
Kufuatia kile ambacho kimetokea usiku wa jana kwa klabu ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, na kueleza hawatashiriki mchezo wa Dabi ya dhidi ya Yanga SC. Kupitia mtandao wa X zamani (Twitter) Rais wa Chama cha WanaSheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi ametoa neno. "Hata kama Simba imezuiwa kucheza ilitakiwa ieleze imechukua hatua gani za kiuongozi kuwasiliana na wahusika baada ya kupuuzwa kwa maelekezo ya Kamishna wa Mchezo. "Huwezi toa tamko kwa umma halafu unaacha maelezo ya msingi na kuishia kusema haki imehifadhiwa ? Ni kukosa umakini je ninyi kama club mumechukua hatua zipi za kusisitiza haki zenu katika kuitaarifu Bodi ya Ligi? au TFF?"
HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Imeanzisha matibabu ya kuziba mapengo Vipandikizi Meno (Dental Implant), ambapo mzizi bandia hupandikizwa kwenye taya, kisha kuwekewa meno juu yake yanayogandishwa na kutumika kama sehemu ya meno yake ya kuzaliwa nayo. Aidha, Serikali imewezesha hospitali hiyo kununua mashine ya kisasa kabisa inayowezesha uchunguzi wa magonjwa ya mifupa ya taya pamoja na CT scan ya uso na kichwa kusaidia kupanga upandikizaji wa vipandikizi vya meno ambapo tangu kununuliwa mwishoni mwa mwaka 2024 tayari wagonjwa 2,251 wamenufaika. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma ya Upasuaji wa hospitali hiyo, Dkt. Rachel Mhaville alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Machi 6, 2025, kuhusu mafanikio ya MNH katika miaka minne ya ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan. Dkt. Mhaville ambaye kwenye mkutano huo alikuwa anazungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa M...
MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69
Valentina Vassilyeva, aliyezaliwa mwaka wa 1707 na kufariki mwaka 1782, anatambuliwa kama "mwanamke ambaye alikuwa na watoto wengi zaidi katika historia" kulingana na Kitabu cha Kumbukumbu cha Guinness. Alikuwa mke wa kwanza wa Feodor Vassilyev, mkulima kutoka Shuya, Urusi. Wakati huo, hapakuwa na mbinu za udhibiti wa uzazi, na kuwa na watoto kulizingatiwa kuwa wajibu wa kidini na kijamii kwa wanawake. Valentina alijifungua mara 27, na kuzaa jozi 16 za mapacha, seti saba za mapacha watatu, na seti nne za watoto wanne, kwa jumla ya watoto 69. Ingawa inaonekana kuwa ya kushangaza, kazi hii ya ajabu imerekodiwa rasmi na kutambuliwa na Guinness World Records. Chanzo: Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness.
BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE
Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania (TPLB) chini ya mwenyekiti wake Steven Mguto imeiomba klabu ya Young Africans Sports Club kusitisha harakati za kufungua kesi katika mahakama ya masuala ya soka duniani CAS kuhusu kuishitumu Bodi hiyo kwa kushindwa kusimamia vyema Sheria na kanuni za Ligi, Bodi ya ligi inaomba klabu hiyo irudi mezani wakae kwa pamoja wamalize mzozo baina Yao Kwa busara na hekima, Bodi ya ligi imekiri Kuna Makosa yalitokea katika kuahirisha Mchezo kinyume na taratibu lakini wanaomba yafanyike majadiliano ya kutafuta Suluhu kwa hekima na busara badala ya kanuni na Sheria, Mpaka kufikia Sasa klabu ya Young Africans Sports Club bado haijatoa ripoti maalumu kuwa kama wapo tayari kufanya majadiliano na Bodi ya ligi.
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMAAA...
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMAAA...
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMAAA...
BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA
# MICHEZO: Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa suala hilo limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha. Akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa, akiamini kuwa suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani. Mnguto ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi. ''Hili jambo lazima hekima na busara itumike, Sheria, kanuni zipo kweli lakini lazima pia utumie hekima na busara, huyo asiyetaka kutumia hekima wala busara kusema kweli huyo hayupo upande wetu kutatua hilo tataizo. Nia yake ni kutengeneza tatizo jipya ambalo haitakuwa na maana yoyote, hata kuziombea timu moja kushushwa daraja unapata faida gani?'' - Steven Mnguto
Comments