DKT. MWAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA AFRITAC EAST

Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam
 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East, iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo.
 
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linaendesha program ya kuongeza ujuzi katika baadhi ya nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Eritri na Malawi.
 
Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Remidius Ruhinduka.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, baada ya mazungumzo yao kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo, mazungumzo yaliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiteta jambo  na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, baada ya mkutano wao kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo, mazungumzo yaliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiongoza mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyochini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira (wa pili kushoto), ambapo walijadili kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE

BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA