MJADALA WA ELIMU - Mrejesho wa Mjadala wa siku 3 wa uboreshaji wa ufundishaji, ujifunzaji na uelewa wa wanafunzi wa Musoma Vijijini
Imebainika kwamba kuna masuala mengi yanayoathiri viwango na ubora wa elimu kwenye shule zetu
Masuala hayo yamegawanyika kwenye maeneo yafuatayo:
(i) Masuala yanayohusu shule
(ii) Masuala yanayohusu wazazi na jamii
(iii) Masuala yanayohusu taasisi/mamlaka za uongozi na utawala (ngazi ya Kijiji, Kata na Halmashauri)
*Vyanzo/vichocheo vikuu 5 vya changamoto hizo vimeainishwa
*Mapendekezo 16 ya utatuzi yametolewa
Ripoti kamili itatolewa wiki ijayo.
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa - Mhe DC Juma Chikoka anaweka msisitizo wa chakula na lishe mashuleni.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumapili, 30 March 2025
Comments