TANESCO YASHINDA TENA TUZO ZA UBORA HUDUMA KWA WATEJA ZA CICM

 📌Urahisi wa upatikanaji huduma kwa njia za kidigitali watajwa moja ya kigezo cha kushinda tuzo hiyo


📌MD Gissima aibuka kidedea kwa Kusimamia Maboresho yenye tija huduma kwa wateja Sekta ya Umma. 


Shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa mara nyingine tena limeshinda tuzo ya the ''Most improved Organization'' eneo la huduma kwa wateja iliyotolewa na Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management(CICM).


Tuzo hizo zimetolewa  28, Machi 2025 jijini Dar es Salaam ambapo Shirika limepata tuzo hiyo baada ya kufanya maboresho ya kutumia njia za kidigitali kurahisisha mchakato wa maombi ya umeme na upatikanaji wa huduma kuwa mwepesi kwa wateja wake.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO , Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Bi  Irene Gowelle  amesema Tuzo hizo ni heshima kwa Shirika ikiwa ni ishara nzuri ya maboresho yanayofanyika kutambuliwa na kuthaminiwa.


‘’ Tuzo hizi ni heshima kubwa kwa TANESCO, zinatuongezea ari ya kufanya vizuri zaidi,tutaongeza ubunifu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wetu’’


Aidha , Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Gissima Nyamo-Hanga na yeye alishinda Tuzo ya heshima ya Kiongozi anayefanya mabadiliko chanya yenye tija upande wa huduma kwa wateja katika Sekta ya Umma.


Tuzo za Tanzania Service excellence awards hutolewa kila mwaka na zinalenga kutambua Taasisi za Umma na binafsi zinazoimarisha na kuboresha huduma bora kwa wateja wake.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE

#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA MJI WA KIHISTORIA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO

BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA

HUU NDIO UKWELI ULIVYO RAFIKI YANGU