Mshambuliaji wa Brazil, Matheus Cunha, mwenye umri wa miaka 25, anasema alikataa ofa za kuondoka Wolves katika dirisha la uhamisho la majira la Januari, lakini amesema amewaambia viongozi wa klabu hiyo kuwa anahitaji "kupiga hatua" kwani anataka "kupigania mataji, kupata changamoto mpya". (Guardian)
Arsenal inaweza kuwa ni nyumbani kwa Cunha, ambaye ana kipengele cha mkataba cha kuuzwa kwa pauni milioni 62.5. Mkurugenzi mpya wa michezo wa Gunners, Andrea Berta, alisaidia kumtwaa mshambuliaji huyo kutoka Atletico Madrid mwaka 2021. (Mail)
Berta pia amekuwa akimfuatiloa kwa muda mrefu mshambuliaji wa Sporting, Viktor Gyokeres, 26 ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanaoonekana kuwa na nafasi kubwa Arsenal inapokuwa inatafuta kuimarisha safu yake ya ushambuliaji. (Athletic)
Kiungo wa AC Milan kutoka Uholanzi, Tijjani Reijnders, anasakwa na Manchester City msimu huu wa kiangazi, ingawa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 hivi karibuni alisaini mkataba mpya ambao haujajumuisha kipengele cha kuuzwa. (Football Insider)
Ajax wanapanga kumrejesha kiungo wa Manchester United kutoka Denmark, Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 33 - ambaye alianza soka la ngazi ya juu la kulipwa huko Amsterdam - atakapomaliza mkataba wake msimu huu. (Manchester Evening News)
Everton inataka kumsajili winga wa Liverpool kutoka Scotland, Ben Doak, mwenye umri wa miaka 19, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Middlesbrough. (Sun)
Manchester United inaweza kuwa na faida katika mbio za kumtwaa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, mwenye umri wa miaka 22 kutoka Ufaransa, kwani ni shabiki wa United tangu akiwa mtoto. (Mirror)
Mwenyekiti wa Ipswich Town, Mark Ashton, alikataa kuweka wazi kuwa mshambuliaji Liam Delap ana kipengele cha kuuzwa kwenye mkataba wake lakini alisema klabu inajivunia kuwa "inalindwa vyema" linapokuja suala la mkataba wa mshambuliaji huyu wa England U21 mwenye umri wa miaka 22. (East Anglian Daily Times)
Bayern Munich hawatarajiwi kumpa mshambuliaji wa Ujerumani, Thomas Muller, mkataba mpya baada ya msimu huu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 anaweza kuhamia Marekani, kwani vilabu vya Major League Soccer vinavutiwa kumchukua. (Sky Sports Germany).
Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen, Simon Rolfes, anasema kocha Xabi Alonso amewaambia viongozi wa klabu kuwa atasalia klabuni hapo, licha ya kuhusishwa na Real Madrid. (Goal).
Comments