Kijiji cha Kataryo ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Tegeruka. Vijiji vingine ni vya Mayani na Tegeruka.
*Sababu zinazohamasisha ujenzi wa sekondari ya Kijiji cha Kataryo:*
(a) Kijiji cha Kataryo kimeshiriki kujenga sekondari za Mugango (Kata jirani ya Mugango), na Tegeruka (Kata ya Tegeruka). Sekondari hizi mbili ziko mbali na Kijiji cha Kataryo kwa umbali wa kilomita kumi (Tegeruka Sekondari), na kumi na tano (Mugango Sekondari)
(b) Mfumo mpya elimu ambao unamtaka kila kijana wa Tanzania kupata elimu ya Kidato cha Nne.
*Harambee ya Mbunge wa Jimbo ya ujenzi wa Kataryo Sekondari:*
Jana, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha Harambee ya kupata fedha na vifaa vya ujenzi wa Kataryo Sekondari. Matokeo yake ni:
(a) Mifuko ya Saruji
*Wanakijiji: Saruji Mifuko 171
*Mbunge wa Jimbo: Saruji Mifuko 200
(b) Michango mingine
*Wanakijiji: Nondo 32
*Wanakijiji: Mchanga tripu moja
*Wanakijiji: Tsh 150,000
*Michango ya fedha kutoka kila kaya itaanza kukusanywa hivi karibuni
KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA SEKONDARI YA KIJIJI CHA KATARYO
Picha zilizoambatanishwa hapa ni za kutoka kwenye tukio la Harambee ya Kijijini Kataryo, Kata ya Tegeruka
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 27 March 2025
Comments